Home Ajira Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025
Ajira

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025
Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025

Matokeo ya Ajira orodha ya majina ya Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliopitia usaili kati ya tarehe 2 Septemba 2024 hadi tarehe 5 Aprili 2025 kuwa:

Matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili.

Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Kuitwa kazini Taasisi mbalimbali za Umma PDF

Hii ni orodha ya walioitwa siku ya leo 11/06/2025

Kupata Barua za Kupangiwa Vituo vya Kazi

Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, barua zao za kupangiwa vituo watazipata kupitia akaunti zao za Ajira Portal, kwenye sehemu ya My Applications.

Mnapaswa kupakua (Download) na kuchapisha (Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi mliyopangiwa.

Maelekezo ya Kuripoti Kazini

Waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliobainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi.

Mnapaswa kwenda na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea, kwa ajili ya kuhakikiwa na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Kwa Waombaji Ambao Majina Yao Hayapo

Waombaji kazi ambao majina yao hayapo katika tangazo hili wanatambua kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili.

Hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi za kazi zitakazotangazwa katika kipindi kijacho.

Soma zaidi: Walioitwa kwenye Usaili Kasulu 2025

1 Comment

  • Nimekuwa muhanga wa Kukosa Ajira Kila mwaka, Tangu nihitimu chuo kikuu Cha Dar es Salaam( DUCE) Fani ya Ualimu mnamo mwaka 2019, na Bado sioni matumaini ya kupata Ajira serikalini hadi sasa ,Naiomba Sekretarieti ya Ajira inifikirie kwa kina kwani hadi sasa, nimekuwa tegemezi kwa familia kitu ambacho sina lugha ya kuzungumza na naogopa kukaa karibu na nyumbani kwa hofu na kwa kuona aibu, najishughukisha na vibarua na shughuli ndogondogo za kujiingizia kipato,ningeomba Sekretarieti ya Ajira chini ya Waziri George Simbachawene inifikirie mimi muhitimu kada ya Ualimu Nina mwaka wa 6 Sasa nikiwa mtaani.

    Hata hivyo katika mwaka huu wa uchaguzi 2025 tulitegemea mabadiliko makubwa katika Sekta ya Ajira lakini bado hatujaonana Dalili zozote kwa Baadhi yetu,
    Usaili nilifanya na nilifaulu Vyema kuingia kwenye Data base( kanzi data) naomba mnifikirie kwani familia yangu inanitegemea kwa udi na uvumba niikomboe kwa Ada iliyonilipia tangu nimeanza msingi Hadi Chuo kikuu.
    Pamoja na hivyo mm ni kijana nina mahitaji mengi yanayoniandama niyafanye, sina mkopo wowote wa kuendesha biashara hadi Sasa.
    Mheshimiwa Waziri na jopo lako naomba tafakari kwa kina maoni yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Wizara ya Afya 13-06-2025
Ajira

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Wizara ya Afya 13-06-2025

Matokeo ya Ajira orodha ya majina ya Walioitwa Kazini Wizara ya Afya...

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Muhimbili 13-06-2025
Ajira

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Muhimbili 13-06-2025

Matokeo ya Ajira orodha ya majina ya Walioitwa Kazini Muhimbili 13-06-2025 Ajira...

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Utumishi 13-06-2025
Ajira

Matokeo ya Ajira Walioitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Utumishi 13-06-2025

Matokeo ya Ajira orodha ya majina ya Walioitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Utumishi...

Matokeo ya Ajira Walioitwa kwenye Usaili Mji Kasulu 2025
Ajira

Matokeo ya Ajira Walioitwa kwenye Usaili Mji Kasulu 2025

Haya hapa matokeo ya ajira na majina ya Walioitwa kwenye Usaili Kasulu...