Sifa za Kujiunga na Vyuo vya Ualimu 2025/2026 WyEST Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) anatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi na Elimu Maalumu kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026.
Kozi zinazotolewa za walimu
- Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 2)
- Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi katika Masomo ya Sayansi na Hisabati (Miaka 3)
Mafunzo haya yatatolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali.
Sifa za Kujiunga na Vyuo vya Ualimu
Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 2)
- Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha Sita mwenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I – III), akiwa na Principal Pass mbili (2).
- Walimu waliomaliza Astashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi pia wanaruhusiwa kuomba.
- Waombaji waliosoma masomo ya Economics, Commerce, na Book Keeping wanapaswa kuomba kozi ya Elimu ya Awali pekee.
- Waombaji waliomaliza Astashahada watapangwa kwenye mikondo kulingana na matokeo yao ya Mtihani wa Taifa.
Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (Miaka 3)
- Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha Nne mwenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I – III).
- Awe na alama ya “C” au zaidi katika masomo matatu, ambapo mawili kati ya hayo yawe ni kati ya yafuatayo:
- Basic Mathematics
- Biology
- Chemistry
- Physics
- Information and Computer Studies au Computer Science
Limetolewa na Wizara ya Elimu Tanzania (MOE)
Utaratibu wa kutuma maombi
- Wanaostahili Kuomba
- Wahitimu wa Kidato cha Nne na Sita
- Walimu waliohitimu Astashahada ya Elimu ya Awali au Msingi
- Maombi kwa Vyuo vya Serikali
- Tembelea mfumo wa udahili wa Wizara kupitia kiungo https://tcm.moe.go.tz
- Uchaguzi wa Kozi
- Mwombaji wa kozi ya miaka 2 atachagua kozi 3 kwa kuanza na ile aipendayo zaidi
- Mwombaji wa kozi ya miaka 3 atachagua tahasusi 3 kwa mpangilio wa upendeleo
- Majibu ya Uteuzi
- Watakaopata nafasi kwenye vyuo vya Serikali watapata majibu kupitia akaunti yao ya mfumo kuanzia tarehe 20/07/2025 na kwenye vyuo walivyochaguliwa
- Waombaji wa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi moja kwa moja kwenye vyuo husika, na majibu yatatolewa na vyuo hivyo
- Fomu za Kujiunga
- Zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara www.moe.go.tz
- Pia zitapatikana kutoka kwa chuo husika baada ya uteuzi
- Maelezo Muhimu ya Mawasiliano
- Waombaji wanatakiwa kuandika:
- Anuani kamili
- Barua pepe
- Namba ya simu inayopatikana kwa urahisi
- Waombaji wanatakiwa kuandika:
Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 10/07/2025.
Soma zaidi: Walioitwa kwenye Usaili Mpwapwa 2025
Leave a comment