Haya hapa matokeo ya ajira na majina ya Walioitwa kwenye Usaili Buhigwe 2025 PDF Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 19-06-2025 hadi 23-06-2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
Ratiba na Maeneo ya Usaili Buhigwe
Usaili utafanyika kwa mujibu wa tarehe zilizotajwa. Kila msailiwa anatakiwa kufika katika muda na eneo aliloainishiwa kulingana na kada aliyoomba.
Kuitwa kwenye usaili Buhigwe 14/06/2025
Walioitwa Halmashauri mbalimbali
Vitambulisho vya Utambulisho
Kila msailiwa Lazima afike na mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Mkazi
- Hati ya Kusafiria
Vyeti vya Kitaaluma
Wasailiwa wote wanapaswa kuja na vyeti halisi kuanzia:
- Cheti cha kuzaliwa
- Kidato cha IV na VI
- Stashahada
- Shahada
Vyeti hivyo vinatakiwa viendane na sifa zilizotajwa kwenye tangazo la kazi.
Maelekezo kwa Kada Maalum
Kada ya Udereva II
Waombaji lazima wawasilishe:
- Leseni ya Daraja E au C
- Cheti cha mafunzo ya udereva kinachothibitisha uwezo wa kupata leseni hizo
Waombaji watakaoshindwa kuwasilisha vyeti hivyo hawataruhusiwa kufanya usaili.
Kada Zinazohitaji Usajili wa Kitaaluma
Waombaji wanapaswa kuwasilisha:
- Cheti halisi cha usajili kutoka Bodi husika
- Leseni ya kufanyia kazi
Nyaraka Zisizokubalika
Nyaraka hizi hazitakubaliwa:
- Testimonials
- Provisional Results
- Statement of Results
- Slips za matokeo ya kidato cha IV na VI
Waombaji watakaowasilisha nyaraka hizi hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
Gharama na Mahitaji Binafsi
Kila msailiwa atajigharamia mwenyewe kwa:
- Chakula
- Usafiri
- Malazi
Uhakiki kwa Waliosoma Nje ya Nchi
Waombaji waliopata elimu nje ya Tanzania wanatakiwa kuwasilisha vyeti vilivyohakikiwa na kuthibitishwa na:
- TCU
- NACTE
- NECTA (kutegemeana na aina ya taaluma)
Namba ya Mtihani
Wasailiwa wameelekezwa kuingia kwenye akaunti zao za ajira kunakili namba ya mtihani, kwani hazitatolewa siku ya usaili.
Hali ya Hewa Buhigwe
Kwa kuwa Iringa ina hali ya hewa ya baridi, msailiwa anashauriwa kuvaa nguo zinazohimili baridi wakati wa kipindi chote cha usaili.
Tofauti ya Majina katika Nyaraka
Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanatakiwa kuwasilisha:
- Hati ya kiapo cha kubadili jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
Waombaji Wasioitwa
Waombaji ambao majina yao hayajaonekana kwenye tangazo hili, watambue kuwa hawakukidhi vigezo vya nafasi husika. Hata hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi zitakapotangazwa tena na matokeo ya usaili yakitoka utayapata hapa.
Leave a comment