Matokeo ya Ajira orodha ya majina ya Walioitwa Kazini Muhimbili 13-06-2025 Ajira Portal 2025 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10-09-2024 na tarehe 18-05-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili.
Walioitwa Kazini Muhimbili
Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
hii ni kwa walioitwa siku ya leo 13/06/2025
Unaweza pitia matangazo mbalimbali ya walioitwa kazini mwezi huu
Kupata Barua za Kupangiwa Vituo vya Kazi
Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, barua zao za kupangiwa vituo watazipata kupitia akaunti zao za Ajira Portal, kwenye sehemu ya My Applications.
Mnapaswa kupakua (Download) na kuchapisha (Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi mliyopangiwa.
Maelekezo ya Kuripoti Kazini
Waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliobainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi.
Mnapaswa kwenda na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea, kwa ajili ya kuhakikiwa na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Kwa Waombaji Ambao Majina Yao Hayapo
Waombaji kazi ambao majina yao hayapo katika tangazo hili wanatambua kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili.
Hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi za kazi zitakazotangazwa katika kipindi kijacho.
Leave a comment