Hatua kwa hatua Jinsi ya kutuma maombi kwenye mfumo wa udahili wa Walimu/Ualimu TCMS 2025/2026 Tembelea Kiunga cha Mfumo kwa kutumia kivinjari (browser) chochote kisha andika kiunganishi (link) cha mfumo wa Udahili na Usimamizi vyuo vya Ualimu https://tcm.moe.go.tz:8081
Baada ya kufungua hiyoo linki, Ukurasa wa nyumbani utafunguka. Kwenye ukurasa wa nyumbani kuna maelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Application status, Pia kuna paneli ya viunganishi vya Mfumo (System links) ambavyo ni Login, Kutengeneza akaunti ya mwombaji (Create Account) Mwongozo wa Udahili (Admission GuideBook) Pomoja na Sehemu ya Kuona Mwongozo wa kutumia mfumo (System Usermanual).
Jinsi ya Kutengeneza akaunti
- Chagua cha Create Account ili kuweza kutengeneza akaunti ya kukuwezesha kuomba chuo.
- Kwenye dirisha ibukizi, Hatua ya 1 ni Usajili wa taarifa za kitaluma kutoka NECTA
- Andika nambari ya kidato cha nne mfano S3610/0052.
- Chagua mwaka uliomaliza kidato cha nne kutoka kushuka chini (drop down)
- Bofya Kitufe cha Register, ukishasajili kwa mafanikio Mfumo utakupeleka hatua ya pili ya usajili.
TCMS User Manual 2025
Na pia fungua kiunganishi kifuatacho uanze kutuma maombi na kuchagua kozi uzipendazo
TCMS Student Portal 2025
Hatua za Kuingiza/Kujaza taarifa Binafsi
- Hatua ya pili ya Usajili ni kujaza taarifa binafisi, Jina, jinsi na namba ya mtihani wa kidato cha nne vitavutwa moja kwa moja kutoka NECTA.
- Itaonyesha (Majina ya mwombaji, Jinsia, nambari ya Kidato cha 4, ongeza nambari ya simu, chagua tarehe ya Kuzaliwa, chagua uraia)
- Ongeza taarifa za Makazi (Anwani ya Mahali, Mkoa na wilaya)
- Ingiza Vitambulisho vya Kuingia (Anwani ya Barua pepe, Nywila na Thibitisha Nywila) Kama inavyoonekana hapa juu kwenye picha
- Bonyeza kitufe cha Usajili, Register.
Jinsi ya Kuhakiki barua pepe
Baada ya Kubonyeza kitufe cha kujisajili yaani Register Utatumiwa kiunganishi (link) kwa ajili ya kuhakiki barua pepe yako ili kukuwezesha kuingia kwenye akaunti yako kwenye mfumo huu wa udahili. Tembelea barua pepe yako, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini, kisha bonyeza kwenye kiunganishi (link) kilichotumwa kwenye barua pepe ili kuweza kuhakiki akaunti yako ambapo itakupeleka kwenye ukurasa wa kuingia kwenye mfumo.
Kuingia kwenye mfumo (login)
Hatua za kufuata ili kuweza kuingia kwenye mfumo.
- Tembelea link ya mfumo https://tcm.moe.go.tz:8081/
- Nenda upande wa wa kulia sehemu imeandikwa System Links
- Bonyenya kwenye Login.
Kutuma maombi au kufanya Udahili
Hatua inayofuata ni kuchagua aina ya tangazo kwa ajili kuomba kozi, Hapa unaweza kuta matangazo Zaidi Zaidi ya moja, lakini unachagua tangazo linaloendana na vigezo vyako, kwa maana kuna kozi zingine zinahitaji matokeo ya kidato cha sita, mengine kidato cha nne. Ili kuweza kuendelea mbele bonyeza Apply.
Ukurasa wa kuchagua Tangazo la Udahili linaonekana, Chagua Tangazo ili uweze kuomba kozi.
Kwa kumalizia, Jinsi ya kutuma maombi kwenye mfumo wa udahili wa Walimu/Ualimu TCMS 2025/2026 mwongozo huu umetupa mwanga juu ya hatua muhimu za kutumia mfumo wa udahili katika vyuo vya ualimu Tanzania.
Kwanza kabisa, Utangulizi umetoa muhtasari wa mfumo huu na umuhimu wake katika kuhakikisha upatikanaji wa walimu wenye sifa.
Hatua za Kujisajili kwenye Mfumo na Kuingia kwenye Mfumo zimefafanuliwa kwa kina ili kuhakikisha watumiaji wanaweza kuanza mchakato wa udahili bila matatizo yoyote.
Aidha, mwongozo umeeleza kwa undani jinsi ya Kufanya Udahili kwa Kuchagua Kozi ya Kusoma Chuoni, hatua ambayo ni msingi wa mafanikio ya mtumiaji katika safari yake ya elimu.
Kwa kuzingatia vipengele hivi, mtumiaji anaweza kutumia mfumo huu kwa ufanisi na kuhakikisha anachagua kozi sahihi katika chuo kinachomfaa.
Soma zaidi: Sifa za Kujiunga na Vyuo vya Walimu 2025
Leave a comment