Walioitwa kwenye Usaili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida 2026

Bonyeza au Gusa KUJIUNGA NASI GROUP LA WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships, Scholarships.

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida anapenda kuwataarifu waombaji kazi za kujitolea zilizotangazwa tarehe 28/04/2026 kuwa usaili unatarajiwa kufanyika tarehe 22/05/2026 saa 02:00 asubuhi. Usaili utafanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwenye Ukumbi wa Mikutano (Morning Meeting).

Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Kufika na vyeti halisi vya Elimu na Taaluma (Original Certificates).
  • Cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
  • Watakaowasilisha hati ya matokeo (Result Slip) au Transcript bila cheti halisi hawatakubaliwa kufanya usaili.
  • Leseni halisi kwa kada zenye leseni.
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Kitambulisho cha Mpiga Kura.

Zingatia:
Wasailiwa wote wanatakiwa kufika eneo la usaili kwa muda uliotajwa.

Pakua PDF ya majina hapa