Haya hapa Matokeo ya Usaili Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Mkwawa (MUCE) usaili wa vitendo Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara huru kilichoanzishwa mahsusi kurahisisha mchakato wa ajira kwa Watumishi wa Umma. Wasailiwa wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia muda na eneo la kufanyia usaili kama ilivyoelekezwa. Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates) pamoja na kitambulisho.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho kwa Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).
Aidha, wanakumbushwa kuwa na vyeti halisi pamoja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Tutorial Assistant Early Childhood Education
- Tutorial Assistant Computer Literacy
- TUTORIAL ASSISTANT ELECTRONICS
- TUTORIAL ASSISTANT PROFESSIONALISM AND ETHICS IN EDUCATION
- TUTORIAL ASSISTANT PRINCIPLES OF EDUCATION
- TUTORIAL ASSISTANT PHILOSOPHY OF EDUCATION
- TUTORIAL ASSISTANT HISTORY
- TUTORIAL ASSISTANT FRENCH TEACHING METHODS
- TUTORIAL ASSISTANT FRENCH LANGUAGE
- TUTORIAL ASSISTANT ECONOMICS
- TUTORIAL ASSISTANT DEMOGRAPHY
- TUTORIAL ASSISTANT COMPUTER SCIENCE
- ASSISTANT LECTURER EDUCATIONAL MANAGEMENT AND LEADERSHIP
Soma zaidi:
Dira
Kuwa Kituo Bora cha Umahiri katika Ajira za Utumishi wa Umma katika ukanda huu.
Dhima
Kutekeleza mchakato wa ajira kwa Watumishi wa Umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwazi na kustahili, pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala yanayohusu ajira.
Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Jukumu kuu la PSRS ni kurahisisha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu cha 29(1), majukumu ya PSRS ni:
- Kutafuta wataalamu mbalimbali wenye ujuzi maalum na kuandaa hifadhidata ya wataalamu hao kwa ajili ya urahisi wa ajira;
- Kusajili wahitimu na wataalamu kwa madhumuni ya urahisi wa marejeo wakati wa kujaza nafasi wazi;
- Kutangaza nafasi za kazi wazi zilizopo katika utumishi wa umma;
- Kuwahusisha wataalamu husika kwa madhumuni ya kuendesha usaili;
- Kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ajira; na
- Kufanya kazi nyingine yoyote au jambo lolote litakaloelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma.
Maadili ya Msingi
Maadili ya msingi ya PSRS ni nguzo za utendaji kazi na mwenendo katika kukabiliana na mabadiliko ya kijamii, kiserikali, kisiasa, na kiteknolojia. Ambayo ni:
- Ufuatiliaji wa umahiri katika utoaji wa huduma;
- Uaminifu kwa Serikali;
- Bidii kazini;
- Uadilifu;
- Heshima kwa wote;
- Kuheshimu sheria; na
- Matumizi sahihi ya taarifa rasmi.
Leave a comment