Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa au kuitwa kwenye usaili TRA 2025 na ratiba katika PDF Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwataarifu wasailiwa wote waliofaulu mtihani wa mchujo na kuchaguliwa (SELECTED) kuwa usaili wa vitendo na mahojiano (Practical and Oral Interviews) utafanyika kuanzia tarehe 02 Mei, 2025 hadi tarehe 14 Mei, 2025.
Waombaji watakaofaulu usaili huo wataajiriwa rasmi.
Wasailiwa wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
1. Kitambulisho cha Utambulisho
Kila msailiwa anatakiwa kuja na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Leseni ya Udereva
- Hati ya Kusafiria
- Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa
Vitambulisho tofauti na hivyo havitatambuliwa. Pia, Matokeo ya usaili wa mahojiano na kuandika yatawekwa hapa.
2. Vyeti vya Kielimu
Msailiwa anatakiwa kufika na vyeti halisi (original) vifuatavyo, kulingana na sifa za nafasi aliyotuma:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Cheti cha Kidato cha IV
- Cheti cha Kidato cha VI
- Diploma (Stashahada)
- Higher Diploma
- Shahada au vyeti vya juu zaidi
HAZITAKUBALIWA:
- Testimonials
- Provisional Results
- Statement of Results
- Form IV na VI Result Slips
Wasailiwa watakaowasilisha vyeti hivyo hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
3. Gharama za Usaili
TRA haitagharamia chochote. Kila msailiwa anapaswa kujigharamia kwa:
- Chakula
- Usafiri
- Malazi
4. Ratiba na Mahali pa Usaili
- Wasailiwa wanapaswa kufika kulingana na tarehe na eneo walilopangiwa kwa mujibu wa ratiba.
- Muda wa kufika ni saa 1:00 kamili asubuhi.
5. Vyeti vya Waliosoma Nje ya Nchi
Wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama:
- TCU
- NACTVET
- NECTA
6. Vyeti vya Usajili kwa Kada Maalum
Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuja na:
- Vyeti vya usajili
- Leseni halali za kufanya kazi
7. Vifaa Visivyoruhusiwa
Msailiwa haruhusiwi kuingia kwenye eneo la usaili akiwa na:
- Simu ya mkononi
- Saa
- Kifaa chochote cha kielektroniki
8. Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi
Kwa taarifa au ufafanuzi zaidi, tembelea ofisi ya TRA iliyo karibu nawe au wasiliana kupitia:
Tovuti: www.tra.go.tz
Simu bila malipo: 0800 780078 / 0800 750075
WhatsApp: 0744 23 33 33
Barua pepe: huduma@tra.go.tz / services@tra.go.tz
Leave a comment